Luke 11:24-26

Kurudi Kwa Pepo Mchafu

(Mathayo 12:43-45)

24 a “Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ 25Naye arudipo na kuikuta ile nyumba imefagiliwa na kupangwa vizuri, 26 bndipo huenda na kuchukua pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza.”

Copyright information for SwhNEN